TAARIFA YA FARAGHA

Inaanza kutumika tarehe 25 Mei 2018.

I. Utangulizi – Sisi ni nani?

Insites Compages NV inajitolea kuheshimu sheria husika ya ulinzi wa data kama ilivyoainishwa katika Kanuni ya 2016/679 kuhusu ulinzi wa watu halisi kwa kuzingatia uchakataji wa data binafsi na kuhusu uhamishaji usio na vizuizi wa data kama hiyo, (hapa baadaye “Sheria ya Jumla ya Ulinzi wa Data” au “GDPR”).

InSites Compages NV, iliyo na ofisi iliyosajiliwa katika Evergemsesteenweg 195, 9032 Ghent (Ubelgiji) na iliyosajiliwa na Crossroads Bank for Enterprises chini ya nambari BE0837.297.070, tanzu na washirika wetu (angalia XIII. Wasiliana kwa maelezo) (hapa baadaye: “InSites”, “yetu”, au “sisi”) inaamini katika kulinda faragha na usiri wa Data Binafsi tunayohifadhi kukuhusu.

Tunafahamu kwamba unaweza kuwa na wasiwasi kuhusu faragha na usalama wa Data Binafsi tunayokusanya, kutumia, na labda kufichua kwa watu wengine kwa madhumuni ya kuturuhusu kudumisha na kutoa bidhaa na huduma zetu. Kutokana na hili, tumeandaa Taarifa hii ya Faragha (“Taarifa”).

Data Binafsi ni mchanganyiko wowote wa maelezo, yanayomilikiwa au yanayo na uwezekano wa kumilikiwa na InSites, ambayo yanaweza kutumika kumtambua mtu binafsi (hapa baadaye “Data Binafsi”). Uchakataji wote wa Data Binafsi na Insites utashughulikiwa kulingana na sheria husika ya ulinzi wa data na Taarifa hii ya Faragha. Maelezo yoyote ambayo hayawezi kutumiwa kumtambua mtu mahususi (kama vile maelezo yaliyojumlishwa ya kitakwimu) sio Data ya Bbinafsi.

Inapaswa kuwa wazi kuwa Taarifa hii inatumika tu kwa uchakataji wa Data Binafsi na InSites kama mdhibiti, na hiyo inamaanisha wakati InSites ndio inayobaini kusudi na njia (“sababu” na “jinsi”) ya uchakataji kama huo.

Taarifa hii inaonyesha jinsi InSites inavyochakata maelezo yaliyokusanywa kupitia

(I) bidhaa na huduma za utafiti wa soko tunazotoa kwa wateja wetu (k.m., ukusanyaji wa maelezo kupitia tafiti, makundi ya watu, jumuiya (kama vile “Square”), mahojiano au aina nyingine yoyote ya zana za utafiti wa soko (hapa baadaye “Shughuli za utafiti wa soko”);

(II) tovuti tofauti kama vile http://www.insites-consulting.com/, https://www.futuretalkers.com/, http://www.howcoolbrandsstayhot.com/ zetu (hapa baadaye “Tovuti”) na shughuli na huduma zote zinazohusiana.

Ikiwa ni lazima tofauti ifanywe kati ya shughuli za utafiti wa Soko na Tovuti zetu.

Pia inaonyesha desturi zetu kuhusu utumiaji wa maelezo kama hayo, hatua tunazochukua kuyalinda, na pia chaguo na haki ambazo wamiliki wa data (“wewe” au “yako”) wanazo kuhusu jinsi tunavyokusanya na kuchakata maelezo yanayowahusu. Wamilki wa data wanaohusika wanaweza kutofautiana kuanzia

(I) washiriki katika shughuli zetu za utafiti wa Soko; au

(II) kila mtumiaji wa Tovuti zetu, waombaji wa kazi, waliojisajili kwa majarida yetu, wateja wa kibinafsi au wa kampuni (na watu wanaohusishwa na wateja wetu wa kampuni), wauzaji (ikiwa ni pamoja na wakandarasi na watu binafsi wanaohusishwa na wasambazaji na wakandarasi wadogo wetu), watu tunaowasiliana nao kwa shughuli za kibiashara (wateja waliopo na wanaowezekana na/au watu wanaohusishwa nao), watu wengine wowote wanaowasiliana nasi

Isipokuwa tutawasiliana nawe vinginevyo, tunafanya kama mdhibiti wa data. Tunapokusanya data binafsi kulingana na makubaliano na watu wengine, na watu hao wengine wabaini njia na madhumuni ya uchakataji, kwa kawaida tunafanya kama mdhibiti wa data kwa niaba ya watu hao wengine ambao watakuwa wadhibiti wa data.

Ikiwa una maoni au maswali yoyote kuhusu Taarifa hii ya Faragha, unaweza kuwasiliana nasi kupitia maelezo yetu ya mawasiliano yaliyotolewa hapo chini ya XIII. Maelezo ya Mawasiliano.

II. Tunachakata Data yako Binafsi vipi?

Sisi ni kampuni ya utafiti wa soko na mshirika wa ESOMAR. ESOMAR ni shirika la kimataifa linalolenga kukuza mbinu bora za utafiti wa soko. Tunazingatia viwango vya kitaalam ambavyo ESOMAR inaweka kwa washirika wake. Pale tunapokusanya na kuchakata maelezo kuhusiana na bidhaa na huduma za utafiti wa soko tunazotoa kwa wateja wetu, wakati huo huo tutalinda faragha ya Data Binafsi tunayopata kutoka kwa washiriki wanaohusika katika shughuli kama hizo.

Tunafanya shughuli hizi kwa niaba ya wateja wetu.

Ambapo tunahitaji kuchakata Data Binafsi chini ya maagizo ya wateja wetu pekee, tunawauliza wateja wetu kutoa maelezo muhimu kwa wamiliki wa data wanaohusika kuhusu utumiaji wake na kama ilivyoainishwa hapo chini. Tunaruhusu wateja wetu kutumia sehemu husika za Taarifa hii au kuzirejelea kwenye Taarifa hii ikiwa wataona inafaa kufanya hivyo. Hata hivyo, hatuwezi kuwajibika ikiwa maelezo haya hayatatosha kuwapa maelezo za yanayofaa.

Tunaweza pia kukusanya na kuchakata maelezo kupitia Tovuti zetu na kuhusiana na shughuli zote za biashara zinazohusiana nayo. Shughuli hizi za uendeshaji zinaweza kuhusisha uchakataji wa Data Binafsi ya watu wafuatao: kila mgeni kwenye Tovuti zetu, waombaji wa kazi, wateja wa kibinafsi au wa kampuni (na watu wanaohusishwa na wateja wetu wa kampuni), wauzaji (ikiwa ni pamoja na wakandarasi wadogo na watu wanaohusishwa na wasambazaji na wakandarasi wadogo wetu.), watu tunaowasiliana kwa shughuli za biashara (wateja waliopo na wanaotarajiwa na/au watu wanaohusishwa nao) au watu wengine wanaowasiliana nasi.

III. Tunakusanya Data yako Binafsi lini?

Data Binafsi inayokusanywa na kuchakatwa na InSites kwa ujumla hupokelewa kutoka kwako kwa hiari, kwa kuzingatia: ushiriki wako katika moja au kadhaa ya shughuli zetu za utafiti wa Soko (kwa mfano dodoso, makundi ya watu au zana yoyote ya utafiti wa soko);

–    ushiriki wako katika moja au kadhaa ya mashindano yetu ya tuzo; na

–    maelezo yote unayotupatia wakati wa ushiriki kama huo.

–    unapowasiliana nasi kupitia Tovuti zetu, kupitia barua pepe, posta, simu, kwa kubadilishana kadi za biashara, kwa kuwasilisha ombi la kutekeleza haki zako,…;

–    unaposhiriki au kudumisha uhusiano wa kimkataba na sisi;

–    unapotuomba kazi;

–    unapojisajili na jarida letu;

–    unapoweka maoni kwenye Tovuti zetu;

–    unapoomba kipakuliwa;

–    Kupitia uvinjari wa tovuti, k.m., unapovinjari Tovuti zetu, tunaweza kukusanya Data Binafsi iliyo na kikomo kupitia matumizi ya vidakuzi kwenye Tovuti zetu.

Ikiwa InSites itapokea Data Binafsi inayokuhusu kutoka kwa wateja au watu wengine na tutumie maelezo haya kwa uchakataji zaidi kama mdhibiti, tutakujulisha kuhusu uchakataji kama huu angalau wakati wa kuwasiliana nawe mara ya kwanza.

Inawezekana kwamba tunapokea Data yako Binafsi kutoka kwa vyanzo vingine, kama vile hifadhidata ya Mteja wetu, orodha ya mawakala, tovuti yetu ya makundi ya watu au kupitia matangazo.

IV. Ni Data gani Binafsi tunayokusanya?

Tunaweza kukusanya na kuchakata Data Binafsi ifuatayo (orodha sio kamili). Kulingana na hali na shughuli za utafiti wa Soko unazoshiriki, hatuhifadhi maelezo yote yaliyotajwa hapa baadaye.

–    Maelezo ya mawasiliano, kama vile jina, anwani ya barua pepe au maelezo mengine yoyote yako muhimu ya mawasiliano

–    Maelezo binafsi na utambulisho, kama vile umri, tarehe ya kuzaliwa, mahali pa kuzaliwa, nakala ya kitambulisho,….

–    Data ya utambulisho wa kielektroniki, kama vile aina ya kivinjari, anwani ya Itifaki ya Intaneti (IP), kitambulisho cha mtumiaji, kitambulishi cha kipekee kinachotolewa kwa kifaa chako, eneo la kijiografia, shughuli zilizofanywa ndani ya ukurasa wa wavuti, maelezo yanayotokana na maudhui kwenye ukurasa wa wavuti,…

–    Historia ya mawasiliano, kama vile mawasiliano yaliyotumwa na yaliyopokelewa (k.m., barua pepe),… kutokana na mawasiliano ambayo tumekuwa nayo wakati wa ushiriki wako.

–    Maelezo yanayohusiana na kazi, kama vile CV, elimu, shughuli za kitaalam, ujuzi wa kitaalam,…

–    Tabia, mapendeleo, maoni au tabia, kama vile tabia ya watumiaji, tabia ya ununuzi, mambo unayopenda kufanya,… kwa ujumla majibu unayotoa kuhusu maswali ya kufanya utafiti wa soko kwa wateja wetu;

–    Picha au rekodi za sauti

Kwa ujumla tunakusanya tu Data Binafsi ambayo inahitajika kutoa huduma zetu kwa wateja wetu na ambayo ni muhimu katika kufikia madhumuni kama ilivyoainishwa hapo baadaye.

Maelezo ambayo tunakusanya kwenye dodoso au kundi la watu yanachakatwa kulingana na kiwango kilichoidhinishwa. Kila mshiriki aliyesajiliwa ana nambari ya kipekee ya utambulisho kwenye hifadhidata yetu ambayo inatuwezesha kukutambulisha kama mshiriki binafsi. Nambari hii itajumuishwa katika nyenzo za siri zinazowasilishwa kwako kama mshiriki huyu binafsi.

Kulingana na madhumuni mahususi ya shughuli za utafiti wa Soko tunazofanya kwa wateja wetu, inawezekana kwamba tunakusanya na kuchakata aina maalum za Data Binafsi (k.m., maelezo ya rangi au asili ya kabila, maoni ya kisiasa, imani ya kidini au falsafa, ushirika wa chama cha wafanyakazi, afya ya mwili au akili, data ya maumbile, data ya bayometriki, mahusiano ya kingono au mwelekeo wa kijinsia). InSites inachakata tu aina maalum za Data Binafsi kwa idhini yako wazi au inapohitajika na sheria.

Pale tunaporuhusu watoto walio chini ya umri wa miaka 16 – au walio na umri wa chini ya hapo, kulingana na masharti yaliyotolewa na sheria za eneo husika – ili kushiriki katika shughuli zetu za utafiti wa Soko mtandaoni, tunafahamu kwamba mbali na idhini ya mtoto lazima tupate idhini inayotolewa au inayoidhinishwa na mtu aliye na jukumu la ulezi wa mtoto. Wakati wa kuchakata Data Binafsi ya watoto, tutaichakata tu wakati tuna idhini kama hizo. Aidha, InSites inaheshimu miongozo inayotolewa na ESOMAR inayohusu ulinzi wa mtandaoni unaohusisha watoto.

V. Sababu na jinsi tunavyotumia Data yako Binafsi?

Kama ilivyoelezwa hapo juu, kwa kawaida tunapata Data yako Binafsi moja kwa moja kutoka kwako. Tunakusanya tu Data Binafsi inayohitajika kwa madhumuni ya kutekeleza huduma au shughuli zetu.
Data Binafsi, inayopatikana kutoka kwa shughuli za utafiti wa Soko inaweza kutumiwa na InSites kwa madhumuni yafuatayo:

–    kwa usajili, mialiko na ushiriki katika huduma zetu za utafiti wa Soko;

–    kwa malengo ya utafiti na kitakwimu;

–    kuunda maelezo mafupi ya pamoja (sio ya watu binafsi);

–    kutuwezesha kuwasiliana na mshindi wa shindano;

–    kutuwezesha kuthibitisha matumizi yako ya nyenzo za siri zilizowasilishwa na sisi kwako; au

–    kutuwezesha kuchukua hatua zinazofaa ikiwa utakiuka majukumu yako kwetu, kama ilivyoainishwa katika sheria na masharti ya kila huduma ya utafiti wa Soko, kama vile jukumu la kutofichua maelezo kuhusiana na nyenzo za siri zilizowasilishwa kwako.
Data nyingine ya Binafsi inayopatikana na InSites (k.m., kupitia Tovuti zetu) inaweza kutumika kwa madhumuni yafuatayo:

–    Madhumuni ya uendeshaji, kama vile: kusimamia na kudhibiti Tovuti, bidhaa na huduma zetu; kuzingatia maombi ya kazi, kujibu maombi ya kutoa maelezo au katika kutekeleza haki zako, usalama, ubora na shughuli za usimamizi wa hatari,….

–    Madhumuni ya kibiashara, kama vile: kutoa bidhaa na huduma zetu; kusimamia, kudhibiti na kuendeleza biashara zetu, mahusiano ya kibiashara, mikataba, bidhaa na huduma; kutoa maelezo kuhusu yanayotuhusu na huduma zetu mbalimbali; kwa malengo ya utafiti na takwimu; kuzingatia masharti yoyote ya kisheria, kanuni au shirika la kitaalam ambalo sisi ni washirika,….

–    Madhumuni ya kibiashara, kama vile: malengo ya uuzaji wa moja kwa moja (k.m., kukutumia jarida letu)

InSites inatumia tu Data yako Binafsi kwa madhumuni haya yaliyotajwa hapo juu, isipokuwa uwe umeidhinisha vingenevyo. Ikiwa tunakusudia kutumia Data yako Binafsi kwa madhumuni mengine tofauti na tuliyowasiliana, tutakujulisha mapema. Kwa mfano: hatutatumia Data yako Binafsi kwa madhumuni ya matangazo isipokuwa uwe umetoa idhini yako wazi na ya mapema.

VI. Tunakusanya Data yako Binafsi kwa sababu gani za kisheria?

InSites huchakata Data yako Binafsi kwa sababu zifuatazo za kisheria:
Kwa shughuli za utafiti wa Soko na majarida: kulingana na idhini yako wazi. Unaweza kuondoa idhini yako wakati wowote. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi unaweza kufanya hivyo, angalia XI. Haki Zako

–    Tunaweza pia kuchakata Data yako Binafsi wakati tuna nia halali ya kufanya hivyo, kama vile kutetea na kushtaki madai na haki za kisheria, na masilahi mengine ya kibiashara. Ambapo tunategemea haki hii ya uchakataji wa kisheria, tutapunguza athari zinazowezekana kwa faragha yako kwa kupunguza matumizi yetu ipasavyo na kuweka hatua za kutosha za ulinzi na usalama ili kuzuia matumizi yasiyoidhinishwa.

–    Uchakataji ni muhimu kwa utekelezaji wa makubaliano ya wateja au wauzaji waliopo (katika kukupa nyenzo za uuzaji zinazohusiana na bidhaa au huduma zinazofanana ambazo umeomba, umetumia au umeshiriki hapo awali) au ili kuchukua hatua zaidi kutokana na ombi lako ili kuingia makubaliano nasi.

–    Tunaweza pia kuchakata Data yako Binafsi wakati tuna jukumu la kisheria la kufanya hivyo.

VII. Tunatumia vidakuzi kwenye Tovuti zetu

Tunatumia vidakuzi, na teknolojia zingine za utambulisho mtandaoni kama vile viashiria vya wavuti, au pikseli ili kuwapa watumiaji hali bora wa utumiaji.

Tunatumia teknolojia hizi kufanya usogezaji katika Tovuti zetu uwe rahisi kwako na kukupa vyema maudhui yanayokufaa.

Tunatumia pia teknolojia hizi kukusanya maelezo ya ufuatiliaji na takwimu kuhusu utumiaji wa Tovuti zetu.

Tunaweza kutumia teknolojia za utambulisho wa mtandaoni kutoka kwa washirika wa uuzaji, tovuti za watu wengine na majukwaa ya mitandao ya kijamii. Teknolojia hizi zinatusaidia kupima ufanisi wa kampeni zetu za uuzaji na uhamasishaji na kuelewa jinsi wageni wanavyofikia Tovuti zetu kutoka kwa tangazo la InSites Consulting.

Unaweza kudhibiti na kusimamia vidakuzi ukitumia kivinjari chako. Tafadhali kumbuka kuwa hatua yako ya kuondoa au kuzuia vidakuzi inaweza kuathiri hali yako ya utumiaji na huenda baadhi ya shughuli zisiweze kupatikana tena.

Vivinjari vingi hukuruhusu uangalie, udhibiti, ufute na uzuie vidakuzi kwa tovuti. Kumbuka kuwa ukifuta vidakuzi vyote basi mapendeleo yoyote uliyoweka yatapotea, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kujiondoa kutoka kwa vidakuzi kwani shughuli hii yenyewe inahitaji kuwekwa kwa kidakuzi cha kujiondoa kwenye kifaa chako.

Kwa maelezo kuhusu vivinjari vya ziada na aina za vifaa tafadhali angalia http:http://www.aboutcookies.org/ au http://www.cookiecentral.com/faq/.

VIII. Tunahifadhi Data yako ya Binafsi kwa muda gani

Tunahifadhi Data yako Binafsi ambayo tunachakata almradi inachukuliwa kuwa muhimu kwa madhumuni ambayo ilikusanywa. Kwa kuzingatia kipindi cha uhifadhi wa data ambacho data binafsi inaweza kuhifadhiwa, inategemea madhumuni ya kukusanya maelezo hayo, kipindi cha uhifadhi wa data kinaweza kutofautiana katika kila hali.

InSites itahifadhi mchakato ufuatao kuhusiana na uhifadhi wa data binafsi iliyokusanywa kupitia utumiaji wa Square:
(i) Baada ya kipindi cha kutotumika cha miezi 4, jukwaa litafungwa. Hii inamaanisha kuwa jukwaa halitaweza kupatikana tena kwa umma.
(ii) Ikiwa jukwaa baadaye (baada ya kufungwa) litakuwa chini ya kipindi kingine cha kutotumika cha miezi 6, jukwaa litawekwa kwenye kumbukumbu na InSites.
(iii) Baada ya kipindi cha kutotumika cha miezi mingine 24 baada ya jukwaa kufungwa kama ilivyoelezwa katika (i), InSites itafuta jukwaa hilo. Hii inamaanisha kuwa data yote (ikiwa ni pamoja na Data Binafsi) itaondolewa na InSites. Isipokuwa kama inahusu data binafsi inayohusiana na vichocheo. Kwa sababu za udhibiti wa kifedha, InSites lazima ihifadhi data hii kwa miaka 7. Insites inajitolea kuweka data hii katika kipindi hiki kwa njia salama (inayobadilika na bila kujali hali ya jukwaa).

Katika tukio ambapo jukwaa litafunguliwa tena, kipindi cha kuwekwa kwenye kumbukumbu na cha ufutaji wa jukwaa hakitaendelea (zaidi). Kila kipindi cha kutotumika kitaanza tena kutoka wakati jukwaa litafungwa tena.

Utaweza kujiondoa kwenye jukwaa wakati wowote. Kuanzia wakati wa kujiondoa, Data yako Binafsi itafutwa ndani ya siku 90 na InSites, isipokuwa kwa Data Binafsi ambayo InSites inahitajika kuhifadhi wakati wa miaka 7 kwa sababu za udhibiti wa kifedha.

IX. Tunachukua hatua gani kuweka kwa usalama Data yako Binafsi

InSites inachukulia usalama wa Data yote Binafsi tunayochakata (k.m., kupitia Tovuti zetu au kuhusiana na shughuli zetu za utafiti wa Soko) kwa uzito. Kwa hivyo tumetekeleza hatua zinazofaa za kiufundi na za kishirika ili kuweka salama uchakataji wa Data Binafsi. Hatua hizi za ulinzi zinatofautiana kulingana na unyeti, muundo, mahali, kiasi, usambazaji na uhifadhi wa Data Binafsi, na zinajumuisha hatua zilizoundwa kulinda Data Binafsi kutokana na ufikiaji usioruhusiwa. Ikiwa inafaa, hatua za ulinzi ni pamoja na usimbaji fiche wa mawasiliano kupitia kwa mfano SSL, usimbaji fiche wa maelezo wakati wa kuhifadhi, kinga mtandao, udhibiti wa ufikiaji, utenganishaji wa majukumu, na itifaki sawa za usalama. Tunadhibiti ufikiaji wa Data Binafsi kwa wafanyakazi wetu na watu wengine ambao wanahitaji ufikiaji huo kwa madhumuni halali na yanayofaa ya kibiashara.

Wafanyakazi, wakandarasi na watu wengine wote ambao watafikia Data yako Binafsi kwa maagizo ya InSites watashurutishwa kuweka usiri na tunatumia vidhibiti vya uwezo wa ufikiaji ili kudhibiti ufikiaji kwa watu ambao wanahitaji ufikiaji kama huo ili kutekeleza majukumu na kazi zao.

X. Uhamisho wa Data Binafsi

Tutashiriki tu Data yako Binafsi na wengine wakati tunaruhusiwa kisheria kufanya hivyo na inapohitajika kutimiza madhumuni yanayohusiana na yale yaliyoelezwa hapo juu.
Tunaposhiriki Data Binafsi na wengine, tunaweka mipangilio ya kimkataba na mbinu za usalama ili kulinda Data Binafsi na kutii viwango vyetu vya ulinzi wa data, usiri na usalama.

Data Binafsi tunayohifadhi inaweza kuhamishwa:

–       kwa wateja wetu

Kwa kutekeleza shughuli zetu za utafiti wa Soko tunakusanya na kuchakata maelezo ya watu binafsi (washiriki) ambao Data Binafsi inaweza kupatikana kuhusiana na kutoa bidhaa na huduma za utafiti wa soko kwa wateja wetu (k.m., wateja waliopo au wanaowezekana wa wateja wetu). Tunachakata maelezo haya kwa niaba ya wateja wetu na hatua ya kushiriki maelezo haya na wateja wetu ni muhimu ili kutoa bidhaa na huduma zetu. Katika muktadha huu inawezekana kwamba tunashiriki picha, rekodi za picha, rekodi za sauti au seti kamili za data tunazohifadhi kukuhusu. Hata hivyo, tutafanya hivyo tu wakati tumepata idhini yako wazi ya uhamishaji huo.

Hatutashiriki Data Binafsi tunayopata kuhusiana na kutoa bidhaa na huduma zetu kwa mteja mmoja, na mteja mwingine. Pia, hatutauza, kukodisha au kukodisha kwa muda mrefu maelezo haya kwa watu wengine.

–       kwa tanzu na washirika wetu

Tunaweza kushiriki Data yako Binafsi ndani ya mtandao wetu wa kimataifa wa mashirika wakati hii ni muhimu ili kutoa au kuboresha bidhaa na huduma zetu (k.m., uchakataji na uhifadhi, kukupa uwezo wa kufikia shughuli na huduma za biashara, kutoa usaidizi kwa wateja, uundaji wa maudhui,…) au wakati hii ni muhimu kwa kusudi ambalo tulikusanya Data yako Binafsi. Kwa maelezo kuhusu tanzu na washirika wetu, tafadhali angalia maelezo ya mawasiliano hapo chini au ubofye hapa.

–       kwa Watoa Huduma wetu

Pale inapofaa, tunatumia watu wengine kutusaidia katika kutoa huduma zetu na kusaidia kutoa, kuendesha na kusimamia mifumo yetu ya ndani ya IT au michakato (ya ndani) ya biashara na kuwaomba wafanye kazi fulani kwa niaba yetu.

Kwa mfano, watoa huduma ya teknolojia ya habari, programu ya wingu kama mtoa huduma, upangishaji na usimamizi wa Tovuti, uchambuzi wa data, programu ya kuajiri, uhifadhi wa nakala ya data, huduma za usalama na uhifadhi.

Tutafichua na kuruhusu tu ufikiaji wa Data Binafsi kwa watoa huduma hawa kwa kiwango kinachohitajika kwa madhumuni husika. Data hii haiwezi kutumiwa nao kwa madhumuni mengine yoyote, haswa sio kwa madhumuni yao wenyewe au ya watu wengine. Aidha, watoa huduma wetu wanashurutishwa kuheshimu usiri wa data yako binafsi kupitia kile kinachoitwa “Makubaliano ya Ulinzi wa Data”.

Unaposhiriki kwenye mfumo wetu wa kutoa vichocheo, huenda tukalazimika kushiriki Data yako Binafsi (k.m. jina, anwani ya barua-pepe,…) na watu wengine ambao hutusaidia kutunza ushughulikiaji wetu wa kutoa vichocheo.

–       mamlaka za utekelezaji wa sheria au mashirika mengine ya kiserikali na udhibiti au kwa watu wengine kama inavyotakiwa, na kwa mujibu wa, sheria au kanuni husika:

Tuna haki ya kufichua maelezo yote na yoyote yanayofaa kwa watekelezaji wa sheria au watu wengine walio na mamlaka ya kupata Data Binafsi, kwa mfano ili kuangalia kama tunatii sheria na kanuni husika, kuchunguza uhalifu unaodaiwa, kuanzisha, kutekeleza au kutetea haki za kisheria. Tutatimiza tu maombi ya kufikia Data Binafsi pale ambapo hii ni muhimu na inafaa na ambapo tunaruhusiwa kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria au kanuni husika.

Sisi ni sehemu ya mtandao wa kimataifa wa mashirika na tunaweza kutumia huduma zinazotolewa na watu wengine au tanzu na washirika wetu katika nchi zingine ili kutusaidia kuendesha biashara yetu. Kutokana na hili, Data Binafsi inaweza kuhamishiwa nje ya washirika wa Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (“EEA”). Katika hali fulani, GDPR inaruhusu InSites kuhamisha Data Binafsi kwenda nchi kama hizo.

Katika muktadha wa utekelezaji wa miradi ya utafiti wa kimataifa, InSites pia inaweza kukualika ushiriki katika miradi ya utafiti wa wateja au washirika wa kibiashara wa kitaifa na wa kimataifa, tena unaojumuisha uhamishaji unaowezekana nje ya EEA.

Kwa kila hali, tumechukua hatua ili kuhakikisha Data yote Binafsi inachakatwa kwa mujibu wa viwango vya kutosha vya usalama na kwamba uhamisho wote wa Data Binafsi nje ya EEA hufanyika kulingana na sheria husika ya ulinzi wa data na kwamba kutakuwa na kiwango kinachofaa cha ulinzi. Tutatekeleza hatua za ulinzi wa kisheria zinazodhibiti uhamishaji kama huu, kama vile vifungu vya muundo vya makubaliano, idhini ya watu binafsi, au sababu zingine za kisheria zinazoruhusiwa na masharti husika ya kisheria.

XI. Haki zako

GDPR inakupa haki fulani kuhusiana na Data yako Binafsi. Haki hizi zimeorodheshwa hapo chini. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa ungependa kutekeleza haki zozote hapo chini. Unaweza kupata maelezo yetu ya mawasiliano chini ya XII. Maelezo ya Mawasiliano, kama ilivyoainishwa hapo chini.
Tafadhali fahamu kuwa hali maalum fulani zinatumika katika kutumia haki hizi, jambo ambalo linamaanisha kuwa huenda usiweze kutumia haki hizi katika hali zote:

a) Uwezo wa Ufikiaji na Mmiliki: Una haki ya kupata data yako binafsi inayoshikiliwa na InSites.

b) Urekebishaji: Unaweza kutuomba turekebishe Data Binafsi isiyo sahihi.

c) Ufutaji (‘Haki ya kusahaulika’): Unaweza kutuomba tufute Data Binafsi katika hali fulani na tutachukua hatua adilifu kuwajulisha wachakataji wa data ambao wanachakata Data Binafsi kwa niaba yetu kwamba umeomba ufutaji wa uhusiano, nakala au urudiaji wowote wa Data yako Binafsi.

d) Vizuizi: Unaweza kuhitaji Data fulani Binafsi iwekewe alama kama inayozuiliwa na pia uzuie uchakataji katika hali zingine.

e) Uwezo wa Kubebeka: Unaweza kutuomba tupeleke Data yako ya Binafsi kwa watu wengine kwa njia ya kielektroniki kama inaruhusiwa chini ya GDPR.

f) Kuwasilisha malalamiko: Unaweza kuwasilisha malalamiko kuhusu uchakataji wetu kwa mdhibiti wa ulinzi wa data, “Mamlaka ya Ulinzi wa Data” (ya Ubelgiji), (anwani) Drukpersstraat 35, 1000 Brussel, (simu) 32 (0)2 274 48 00, (barua pepe) contact@apd-gba.be.

Aidha, chini ya hali fulani, una haki ya:

–     ambapo uchakataji unategemea idhini, kuondoa idhini; majarida yote yanajumuisha kitufe cha kujiondoa katika kijachini cha barua pepe hiyo.

–     kupinga uchakataji wowote wa data ya binafsi ambayo InSites imethibitisha msingi wa kisheria wa “masilahi halali”, isipokuwa sababu zetu za kutekeleza uchakati huo zinazidi upendeleo wowote kwa haki za faragha za mtu binafsi; na

–     kupinga uuzaji wa moja kwa moja (ikiwa ni pamoja uchanganuzi wowote kwa madhumuni kama hayo) wakati wowote

XII. Masasisho ya Taarifa hii

InSites ina haki ya kurekebisha na kusasisha Taarifa hii wakati wowote. Tarehe ya sasisho la mwisho inaweza kupatikana juu ya Taarifa hii.

Kwa hivyo, unapaswa kukagua Tovuti zetu mara kwa mara ili upate taarifa kuhusu sera na desturi zetu za sasa.

XIII. Maelezo ya Mawasiliano

Ikiwa una maoni au maswali yoyote kuhusu Taarifa hii ya Faragha au kuhusu uchakataji wa Data yako Binafsi na InSites kama mdhibiti wa data, unaweza kuwasiliana nasi

–      Kupitia barua pepe: info@insites-consulting.com

–      Kupitia simu: +32 (0)9.269.15.00

–      Kupitia barua ya posta:

InSites Compages NV (BE)
Evergemsesteenweg 195
9032 Ghent
Belgium
BE0837.297.070

InSites NV (BE)
Evergemsesteenweg 195
9032 Ghent
Belgium
BE0465.109.357

InSites Consulting BV (NL)
Barbizonlaan 45
2908 ME Capelle aan den IJssel
The Netherlands
NL822.105.469.B01

InSites Consultants Ltd. (UK)
27/31 Clerkenwell Close, unit 5.14
EC1R 0AT London
United Kingdom
GB994.9938.26

InSites Marketing Consulting Inc (US)
1410 Broadway, Suite 3001
New York, NY 10018
United States
61-1661807

InSites DE GMBH (DE)
Factory Campus – Erkrather Strasse 401
40231 Düsseldorf
Deutschland
DE314171417

ISC Reasearch SRL (ROM)
2 Strada Dr. Liviu Gabor
300057 Timisoara
Romania
RO28395601

Direction First Pty Ltd (AUS)
241 Castlereagh Street, Level 5
Sydney, NSW 2000
Australia
ACN 078348320

InSites Bangkok
Asia Centre Building, #28-119, – 173 S Sathorn Rd, Thung Maha Mek, Sathorn
10120 Bangkok
Thailand

InSites Bogotá
Provokers Colombia – Calle 93 No. 15-40 piso 2
Bogotá
Colombia

InSites Buenos Aires
Provokers Argentina – Av. Costanera R. Obligado 4899
1426 Ciudad Autónoma de Bs
Argentina

InSites Hong Kong SAR
31-32/F, Hysan Place – 500 Hennessy Road
Causeway Bay, Hong Kong SAR
People’s Republic of China

InSites Jakarta
WeWork Revenue Tower, 27th Floor Room 101 – Jl. Jend. Sudirman No. 52-53, RT.5/RW.3
12190 Jakarta
Indonesia

InSites Johannesburg
Glasgow House – 54 Peter Place, Peter Place Office Park
2191 Bryanston
South Africa
VAT: ZA4150251587

InSites Manchester
The Hive – 51 Lever Street
M11FN Manchester
United Kingdom

InSites Manila
9/F, WeWork, Uptown Bonifacio Tower Three – 36th St. Corner 11th Ave
1634 BGC, Taguig City
Philippines

InSites Mexico City
Provokers México – Melchor Ocampo 193 Torre Privanza piso 15 Col. Verónica Anzures C.P
11300 Ciudad de México
México

InSites Montevideo
Provokers Uruguay –
Montevideo
Uruguay

InSites Paris
88 Avenue Charles de Gaulle
92200 Neuilly-sur-Seine
France

InSites Rotterdam
Watermanweg 40-42
3067 GG Rotterdam
The Netherlands
VAT: NL822.105.469.B01

InSites Santiago
Provokers Chile – Avenida Los Dominicos 8630, suite 403
Las Condes, Santiago
Chile

InSites Santo Domingo
Provokers Dominican Republic – Calle Haim López Penha #21, Edificio Prieto Nouel 4to piso, Ensanche Paraíso
Santo Domingo
Dominican Republic

InSites Sao Paulo
Provokers Brazil – Av. Brigadeiro Faria Lima, 201 – Cj
271 Sao Paulo
Brazil

InSites Seoul
WeWork, Gwanghawamun Room 126, 2/F – 50 Jong-ro 1-gil Jongno
03142 Seoul
South Korea

InSites Shanghai
5th Floor Room 128 – 819 Nanjing Road West, Jing’an District
200041 Shanghai
People’s Republic of China

InSites Singapore
71 Robinson Road #14-01
068895 Singapore
Singapore

InSites Taipei
4F, No 120, Sec. 2, ChienKuo N. Rd.
10483 Taipei
Taiwan